Mheshimiwa CP-Suzan S.Kaganda, Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, ametoa wito wa kutunza maadili ya Kitanzania Pamoja
na umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania waliopo nchini Zimbabwe. Wito huo, umetolewa wakati wa hafla fupi ya
kuwakaribisha vijana/wanafunzi kutoka nchini Tanzania ambao wapo nchini Zimbabwe kwa ajili ya masomo katika Chuo
Kikuu cha Afrika(Africa University) kilichopo mjini Mutare-Zimbabwe. Hafla hiyo, imeandaliwa na diaspora wa Tanzania
wanaoishi mjini Mutare, Zimbabwe.
Aidha, Mheshimiwa Balozi Kaganda, amewataka wanafunzi hao kuzingatia kilichowaleta na sio kujihusisha na vitendo vya
uvunjifu wa maadili, sheria, na taratibu za nchi mwenyeji. Pia, amewataka wajitahidi kulinda taswira nzuri ya Tanzania
kimataifa.Kwa upande wao, wanafunzi hao wamemshukuru Mheshimiwa Balozi na timu ya maafisa kutoka Ubalozini ambapo
wameahidi kuendelea kuwa Mabalozi wazuri huku wakizingatia masomo yao vizuri.






