Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Emmanuel Tutuba na ujumbe wake wametembelea Ubalozi wa Tanzania, Harare-Zimbabwe. Ziara hii imwefanyika wakati Gavana Tutuba na Ujumbe wake wakiwa ziarani nchini Zimbabwe kushiriki Mkutano wa Macroeconomics Financial Management Institute of Eastern and Southern Africa Executive Committee Meeting uliofanyika mjini Harare.
Katika ziara hiyo Gavana Tutuba alishukuru Ubalozi kwa mapokezi waliyoyapata na kuzishukuru ofisi za Balozi za Tanzania nje ya nchi kwa mchango mkubwa zinaoutoa katika utekelezaji wa sera ya Diplomasia ya Uchumi kwa kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini na kuongeza kawa, Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini ili kuvutia zaidi wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.