Tarehe 22 Agosti, 2025, Mheshimiwa Balozi Suzan S. Kaganda alikutana na Mheshimiwa Jenerali Mstaafu Peter A.L. Namathanga, Balozi wa Jamhuri ya Malawi nchini Zimbabwe na kujadiliana masuala mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Malawi.
Katika mazungumzo hayo pamoja na masuala mengine pande zote mbili zilikubaliana kuwasiliana na mamlaka husika kwenye nchini kwao ili kuwezesha kufanyika kwa Mkutano wa Sita wa JPC kati ya Tanzania na Malawi ambapo kwa mkutano huu nchi ya Malawi ndio itakuwa mwenyeji.
Mhe. Balozi Namathanga alimshukuru Balozi Kaganda kwa mazungumzo hayo na kuahidi kufuatilia masuala yote yaliyojitokeza ili kuendelea kukuza ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya Tanzania na Malawi.