BALOZI wa Tanzania Nchini Zimbabwe, IGP Mstaafu Simon SIRRO, amewakaribisha Watanzania kuwekeza nchini Zimbabwe na kusema kuwa fursa ni nyingi na kuwataka watu wachangamkie fursa. Akizingumza ubalozini jijini Harare, Balozi SIRRO amezitaja fursa zilizopo nchini humo ni pamoja na Lugha ya Kiswahili, Biashara ya usafirishaji na biashara kadhaa za uuzaji wa bidhaa ambazo wananchi wa zimbabwe huzinunua nchini Tanzania hususani Kariakoo ambapo Balozi SIRRO amehamasisha Watanzania kwenda Harare, Bulawayo na miji mingineyo kwenda kuwekeza kutoa huduma kadhaa ikiwemo maduka ya jumla. Balozi SIRRO pia ameeleza namna ofisi yake inavyoshughulika kualika wawekezaji kutoka nchini humo kuja kuwekeza Tanzania. Wakati huo huo Balozi SIRRO alipata nafasi ya kwenda kushuhudia darasa la Somo la kiswahili ambapo wananchi wa Zimbabwe wanajifunza somo hilo.
