Mheshimiwa CP-Suzan S. Kaganda, Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe amepokea ujumbe wa Mheshimiwa Laurent Luswetula (Mb), 
Naibu Waziri wa Fedha na Mheshimiwa Dkt.Pius Chaya (Mb), Naibu Waziri-Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, ambao wapo nchini Zimbabwe kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Mawaziri wa SADC wa Sekta za Fedha,
Afya na Uwekezaji unaofanyika mjini Harare,nchini Zimbabwe.
Mkutano huo wenye kaulimbiu ya "Advancing Industrialisation, Agricultural Transformation & Energy Transition for a
Resilient SADC" utawakutanisha Maafisa Waandamizi na Wataalam kutoka sekta hizo ili kujadili namna bora ya kuleta
mabadiliko chanya kwenye sekta hizo kwa nchi wanachama wa SADC.