Mheshimiwa CP-Suzan Kaganda, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Zimbabwe amekutana kwa Mazungumzo na Eng. Moses Nyoni, Mtanzania
anayeishi na kufanya kazi nchini Zimbabwe kwenye taasisi ya Southern African Railway Association (SARA) yenye ofisi zake nchini Zimbabwe.


Katika mazungumzo hayo, Mheshimiwa Balozi Kaganda amempongeza Bw. Nyoni kwa kupata fursa ya kufanyakazi na taasisi hiyo na kumsisitiza kuhakikisha kuwa anakuwa mwakilishi mzuri wa taswira ya Tanzania kwenye taasisi hiyo ya Kimataifa. Aidha amemtaka kuona namnagani Reli ya tazara na Bandari za Tanzania zitaongeza ufanisi kwenyekata ya usafirishaji hususan kwa Zimbabwe kwani tayari tuna ofisi za Bandari hapa Harare na Zambia.

Aidha, amemtaka Eng. Nyoni kujitahidi kuhakikisha kuwa Tanzania inanufaika na uwepo wake kwenye taasisi hiyo katika sekta ya miundombinu ya reli.
 
Kwa upande wake Eng. Nyoni ameshukuru na kuahidi kufanyikia kazi maono ya Ubalozi, kwani yanalengo la kutekeleza na kukuza Diplomasia ya Uchumi.