Mheshimiwa CP- Suzan S. Kaganda, Balozi wa Tanzania nchini Mauritius, mwenye makazi yake mjini Harare, nchini
Zimbabwe, amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Mheshimiwa Dharambeer Gokhool, G.C.S.K, Rais wa Jamhuri ya Mauritius,
kwenye Ikulu ya nchi hiyo iliyopo Reduit-Mauritius.
Baada ya kuwasilisha Hati hizo, Mheshimiwa Balozi alikuwa na mazungumzo na Mheshimiwa Rais Dharambeer ambapo pamoja
na masuala mengine, Mheshimiwa Rais Dharambeer amempongeza na kumkaribisha Mheshimiwa Balozi Kaganda kwenye eneo
hilo la uwakilishi na kumuhakikishia ushirikiano kutoka kwa Serikali ya Mauritius katika kipindi chote cha utekelezaji
wa majukumu yake.
Kwa upande wake, Mheshimiwa Balozi Kaganda ameshukuru kwa mapokezi hayo na kuahidi kushirikiana na Serikali ya Mauritius
ili kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia uliopo kati ya nchi hizi mbili pamoja na kukuza sekta za biashara, uwekezaji,
utalii na Uchumi wa Buluu kwa maendeleo ya nchi zote mbili.









