Mhe. Suzan Kaganda, Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, ameshiriki katika Mkutano wa Mawaziri wa Fedha
na Afya wa SADC akimuwakilisha Mhe. Mohamed Mchengerwa (Mb), Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, na kujadili masuala mbalimbali ya Afya ikiwemo mpango wa Ununuzi wa Pamoja wa Bidhaa
za Afya katika Ukanda wa SADC na Ugharamiaji wa Sekta ya Afya.





