Ujumbe wa Tanzania Ulioongozwa na Mhe. Joyce Ndalichako Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu ulishiriki Mkutano wa Majadiliano ya Utatu wa Viongozi wa Ngazi ya Juu kuhusu Masuala ua Uhamiaji na Nguvu Kazi katika Ukanda wa Nchi Wanachama wa SADC tarehe 29-30 Novemba, 2022, Victoria Falls, Zimbabwe.

 

Kwa upande wa Tanzania wa Tanzania katika mkutano huo Mhe. Prof. Ndalichako aliambatana na Naibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Isaac Maduhu, Naibu Katibu Mkuu- TUCTA;Kanali Lucas Magembe,kutoka ATE Bibi. Mercy Patric; kutoka Chama cha Wafanyakazi Zanzibar, Mwanamkuu Gharib Mgeni na Ofisi ya Waziri Mkuu, Joseph Nganga pamoja na Eliud Ikomba kutoka Idara ya Uhamiaji.